Na Elinipa Lupembe.
Watoto halmashauri ya Arusha, wamewataka wazazi kutambua na kuheshimu haki zao, kwa kuacha kuwafanyia vitendo vya ukatili, vitendo ambavyo vinakatisha ndoto za maisha ya watoto wengi, pamoja na kuathiri maisha yao kisaikolijia.
Watoto hao wamewasilisha vilio vyao, kupitia jumbe mbalimbali walizoziwasilisha kupitia sanaa ya ngoma, nyimbo, mashairi, ngonjera na mashairi, wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, yaliyofanyika kewenye viwanja vya shule ya msingi Musa iliyoko kata ya Musa.Namnyaki Mollel, mwanafunzi wa darasa la tano, shule ya msingi Nengung'u, ameweka wazi kuwa watoto wengi hufanyiwa ukatili na watu wao wa karibu, ambao huishi ndani ya famili na jamii zetu, tunaomba wazazi kuachana na mila potofu inayoruhusu mtoto kuozeshwa katika umri mdogo, tabia ambayo imejengeka kwenye jamii yetu.
"Tunaomba wazazi wetu, kuachana na mila na desturi potofu, zinazochangia vunjifu wa haki za watoto, tunaomba wazazi wetu msituozeshe katika umri mdogo, lakini pia wazazin hakikisheni kila mtoto anapata haki zake za msingi zinazomuwezesha mtoto kupata makuzi bora" amesisistiza Namnyaki.
Aidha watoto hao, wameiomba serikali kulinda haki zao, kwa kusimamia kesi za watoto, waliofanyiwa ukatili, kesi ambazo mara nyingi humalizika bila kupata suluhisho na kwanyima haki watoto wengi.Naye mgeni rasmi, akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji, Mwanasheria wa halmashauri ya Arusha, Monica Mwailolo amewakumbusha wazazi na jamii, kufanyia kazi malalamiko yaliyowasilishwa na watoto, na kuwasihi wazazi kuachana na mila na desturi zinazowafanyia ukatili watoto kwa kuhakikisha kila mzazi anatekeleza jukumu lake katika malezi.
"Wazazi mna jukumu kubwa la kutekeleza haki za watoto, na kuwalinda watoto, kama wazazi mataacha kuwaozesha watoto katika umri mdogo, kuwakeketa na kuwatelekeza, tutakuwa na jamii yenye kutekeleza, haki za watoto kufuatia agenda 2040 kama ilivyo kauli mbiu ya kuifanya Afrika inayotekeleza Haki za watoto 2040" amesistiza mgani rasmi huyo.
Aidha umeainishwa ukatili unaofanya dhidi ya watoto ni pamoja na ndoa za utotoni, kukeketwa, kubakwa na kulawitiwa, kufanyishwa kazi, pamoja na kutelekezwa na kuwasisitiza jamii, kusimamia na kupambana dhidi ya ukatili huo, unaofanywa na jamii kwa watoto.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila tarehe 16.06 ya mwaka, halmashauri ya Arusha imeungana na mataifa 51 duniani kuadhimisha siku hiyo maalum, kwa kushirikaiana na wadau wa mashirika ya ACE AFRICA, CWCD, COMPASSION, DORCAS AID, KIZAZI KIPYA, ELCT - KKP, maadhimisho yaliyobeba Kauli Mbiu "Tutekeleze Ajenda 2040: Kwa Afrika inayolinda Haki za Mtoto.
PICHA ZA MATUKIO.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.