• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Watoto wa Kimnyaki wapinga adhabu kali dhidi yao na kuitaka jamii kuacha kutoa adhabu kali kwa watoto

Posted on: November 13th, 2018

Watoto wa kata ya Kimnyaki, halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru, wamefanya mdahalo na kujadili juu ya kuondolewa kwa adhabu kali kwa watoto nyumbani na shuleni, mdahalo uliofanyika kwenye ofisi ya kijiji cha Kimnyaki mapema mwishoni mwa wiki iliyopita.


Mdahalo huo uliokuwa na mvutano mkubwa na wa aina yake, ulitoa fursa kwa pande mbili kupinga kwa hoja, huku upande mmoja ukitaka adhabu kali ziondolewe shuleni na upande unaopinga na kutaka adhabu hizo ziendelee kwa kuwa zinafundisha.


Licha ya kuwa, pande zote mbili zilijenga hoja zake vizuri, lakini mjadala huo ulihitimishwa, kwa watoto hao kuwataka wazazi, walezi, walimu na jamii kwa ujumla, kuacha tabia ya kutoa adhabu kali kwa watoto na kuainisha madhara wanayoyapata watoto, wanapopewa adhabu kali ambazo wakati mwingine huwasababishia hadi vifo.


Zaidi watoto hao, wameonesha kukerwa na kusikitishwa na baadhi ya walimu, wazazi na walezi wanaowaadhibu watoto licha ya kuwasababishia, kuathirika kisaikolojia wengine hupata maumivu makali, ulemavu, makovu yasiyo kwisha maishani na hata wengine kufa.


Watoto hao walitaja kwa hisia, adhabu ambazo watoto hupewa wawapo shuleni ni pamoja na kuchapwa fimbo zisizo na idadi, kuchimba visiki, kulima eneo kubwa, kusomba na kupasua mawe jambo ambalo huwafanya wanafunzi kuumia kimwili na kiakili na kushindwa kujiamini kabisa na kujiona kama wahalifu.


Wameeleza kuwa, watoto wanapopewa adhabu, wanajenga uwoga , wasiwasi, ukatili na kushindwa kabisa kujiamini mbele ya jamii, huku wengine wakiamua kukimbia nyumbani na kwenda kuishi kwenye magenge ya wahuni na kuzurura mitaani.


Wametoa rai kwa wazazi, walezi na walimu kuwa na tahadhari ya kuwa na taifa la watu wasiojiamini hapo baadae na kufafanua kuwa, ili kunusuru taifa letu lisifike huko, ni kuwa na tabia ya ukaribu na watoto wao, kujenga tabia ya kuwasikiliza maoni yao kwa upendo, kuwajali pamoja na kuwavumilia, kwa kuwa kukosea ni sehemu ya makuzi ya mtoto, inayomuwezesha mtoto kujengeka katika misingi iliyo bora na imara.


Hata hivyo wameiomba jamii kuacha tabia ya kuwaadhibu wakiwa na hasira kali, badala yake, kukaa na kuzungumza na watoto hao, juu ya makosa waliyoyafanya na kuwafahamisha madhara yanayoweza kuyapata pindi wanapofanya makosa hayo.

Naye Mkuu wa shule ya sekondari Kimnyaki, mwalimu Daniel Sulumo, amehitimisha mdahalo huo kwa kusema kuwa, licha ya kuwa adhabu, hutumika kama kichocheo cha kurekebisha tabia ya mtoto na kumfanya kuenenda kwa kufuata taratibu lakini amesisitiza zaidi jamii kuacha tabia ya kutoa adhabu kali zilizozidi kiasi, kwa kuwa adhabu kali zina madhara makubwa kwa watoto hata katika maisha yao ya baadae.

Amewataka wazazi, walezi na walimu kutumia muda mwingi, kuzungumza na mtoto pindi anapokosea na kumuelewesha madhara ya kosa hilo pamoja na kumtaka kueleza jambo lililomsababisha kufanya kosa hilo.


"Mtoto akifanya kosa anatakiwa kurekebishwa kwa namna nyingi, unaweza zungumza nae na kumuelewesha madhara ya kosa alilolifanya, na kabla ya kumuadhibu lazima kwanza afahamu kosa lake, eleze sababu za yeye kufanya kosa na akubali adhabu unayompa" amesema mwalimu huyo.


Mdahalo huo, umefanyika kwa ushirikiano wa halmashauri ya Arusha na wadau wa mashirika ya 'Centre for Women and Children Development'- (CWCD) chini ya mradi wa Sauti Yangu na kusimamiwa na Jukwaa la Haki za Watoto (Tanzania Child Right Forum - TCRF) chini ya ufadhili wa 'Child Fund Korea', mdahalo wenye lengo la kuwajengea watoto uwezo wa kujiamini na kujitambua huku wakiwa na uwezo wa kujenga hoja na kuzitetea pamoja na kuzungumza mbele ya watu bila hofu wala woga.

 

PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA  MDAHALO HUO

Kundi la watoto kutoka katika jamii ya Kimnyaki, wakifuatilia mdahalo juu ya adhabu kali dhidi ya watoto, ikiwa upande wao ukitaka adhabu kali shuleni zisifutwe.



Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kimnyaki, wakati wa mdahalo juu ya adhabu kali dhidi ya watoto, ikiwa upande wao ukitaka adhabu kali shuleni zifutwe.



Mkuu wa shule ya sekondari Kimnyaki mwalimu Daniel Sulumo, akihitimisha mdahalo juu ya adhabu kali dhidi ya watoto zifutwe. 






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.