Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi, amewaongoza waombolezaji wakiwemo, viongozi wa Chama na Serikali, Waheshimiwa Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Arusha kwenye Ibada maalum ya kuaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa Idara ya Kilimo, halmashauri ya Arusha, Marehemu Paulus Barnabas Kessy, Ibada iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu eneo la Moshono Suye jijini Arusha.
Mara baada ya kukamilika ibaada ya hiyo leo, mwili wa Marehemu utalala kwenye hospitali ya mkoa Mount Meru na kesho utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Moshi Vijijini -Kirua Vunjwa mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
"Bwana alitoa Bwana ametwaa jina lake Lihimidiwe"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.