• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Watumishi Arusha DC watakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma

Posted on: October 8th, 2018

Watumishi wa halmashauri ya Arusha, wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ya kuwahudumia wananchi na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma,  ili kuleta tija na maendeleo katika halmashauri hiyo.

Akizungumza na watumishi hao, alipokutana nao kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, amesema kuwa, jambo kubwa litakalosaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wa halmashauri ya Arusha ni uwajibikaji wenye tija na moyo wa kujituma bila kuchoka.

Dkt.Mahera ameongeza kuwa, jukumu kubwa la watumishi wa umma ni kuwahudumia wananchi bila kujali hali zao wala itikadi zao, kwa kuwa ni haki ya kila mwananchi kupata huduma bora anayohitaji, hali ambayo itajenga imani kwa wananchi.

 " Kila mwananchi anahaki ya kuhudumiwa na kupata huduma bora na sahihi anayohitaji bila kujali hali yake ya kiuchumi, itikadi zao za kidini wala za kisiasa" amesisitiza Mkurugenzi Mahera.

Hata hivyo, Dkt. Mahera amewataka wakuu wa Idara na Vitengo, kuwasimamia watumishi wote walio chini yao na kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya pamoja na kusimamia miradi yote ya maendeleo, inayotekelezwa chini idara na vitengo vyao bila kutoa wala kupokea rushwa.

"Niwatake wakuu wote  wa Idara na Vitengo,  kuwajibika vizuri na kuhakikisha mnawasimamia watumishi walio chini yenu huku mkisimamia vyema miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Idara na Vitengo vyenu, na kuacha tabia ya kupokea rushwa" amesema Dkt.Mahera

Kadhalika, Mkurugenzi Mahera, amemtaka Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo, kuhakikisha kila  idara inatekeleza majukumu yake kwa ufasaha pamoja na kutenga muda maalumu wa kusikiliza matatizo ya wananchi.

Kwa upande wake Afisa Utumishi  wa halmashauri ya Arusha, Mohammed Mavura,  ameahidi kushirikiana na watumishi wa ngazi zote ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kuleta maendeleo katika halmashauri yao.

Afisa Utumishi huyo pia, amewataka watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano huku nidhamu ya kazi ikiwa ni kipaumbele na kuongeza kuwa, Idara ya Utumishi haitawahurumia, watumishi ambao hawatatekeleza majukumu yao vizuri kwa mujibu wa sheria za kazi.

"Nitakuwa mtu  wa kwanza kumshauri mkurugenzi kumshughulikia mtumishi yeyote ambaye, hatatekeleza majukumu yake  ipasavyo" amesema Mavura

Halmashauri ya wilaya ya Arusha ni moja kati ya halmashauri yenye mkakati wa kutekekeza kwa vitendo, juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii, kupiga vita rushwa pamoja na kutoa huduma kwa kuzingatia haki sawa kwa wananchi wote.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.