Na. Elinipa Lupembe.
Watumishi wa makao makuu halmashauri ya Arusha (ARUDHA DC HQ) wameridhishwa na kupongeza agizo la mkuu wao wa wilaya ya Arumeru, la kupanga siku ya Alhamisi kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka ofisi zao, jambo ambalo licha ya kuweka mazingira safi lakini pia linaongeza ushirikiano baina ya watumishi na kuleta hamasa katika utekelezaji wa kazi za kiutumishi.
Wakizungumza wakati wa kufanya usafi asubuhi ya leo, watumishi hao wameweka wazi kuwa, zoezi hilo la kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka ofisi zao ni la muhimu sana kwao, hasa kwa kuzingatia wahudumu waliopo ni wachache hawana uwezo wa kumudu kufanya usafi na kufikia maeneo yote kwa wakati, hivyo zoezi hilo limewezesha mazingira yetu kuwa safi.
Afisa Utumishi halmashauri ya Arusha, Elizabeth Ngobei, amesema kuwa, watumishi wameridhishwa na kujitoa kwa suala la kufanya usafi wa mazingira ya ofisi zao, kwa kuwa, licha ya mazingira kuwa safi lakini pia linakutanisha watumishi pamoja na kuongeza umoja baina yao huku likiongeza ufanisi katika kazi.
Naye Afisa Afya halmashauri ya Arusha, Issa Msumari, amethibitisha umuhimu wa watumishi kufanya usafi wa mazingira yao, unajenga umiliki wa maeneo yao, unaleta hamasa kwa wananchi kujituma kufanya usafi, na zaidi linaongeza tija na ufanisi katika kazi.
"Kufanya usafi wa eneo unapofanyia shughuli yoyote ni jukumu la kila mtu anayehusika na eneo hilo, hivyo hata sisi watumishi ni jukumu letu kufanya usafi katika maeneo yetu, hii inahamasisha hata wananchi wetu kuiga mfano kwa kufanya usafi kwenye ameneo yanayowazunguka" amethibitisha Afisa Afya Msumari.Aidha watumishi hao, wameshauri kuwa ili zoezi la usafi liwe la ufanisi zaidi, ni vema uongozi kuwaandalia vifaa vya kutosha vya kufanyia usafi, ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi, amewapongeza watumishi wote kwa mapokeo chanya ya kufanya usafi wa mazingira na kuwataka watumishi wa hngazi zote kuahkikisha kila siku ya Alhamahi wanatumia muda wa saa mbili za asubuhi, kufanya usafi wa maeneo yanayizunguka ofisi za Umma na kuahidi uwepo wa vifaa vya kutosha wakati wa zoezi hilo.
"Ninawapongeza watumishi wote kwa kufanya usafi wa mazingira, katika maeneo yote yanayozunguka ofisi za makao makuu ya halmashauti yetu, zoezi hili ni endlelevu na niwaahidi uwepo wa vifaa kila wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo" amesema Msumi.
Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, aliagiza watumishi wote wa halmashauri za wilaya hiyo Meru na Arusha, kuwa na zoezi endelevu la kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka ofisi zao kuazia ngazi ya kijiji,,kata na halmasahuri, kila siku ya Alhamisi lengo likiwa ni utekelezaji wa agizo la mheshimiwa Makamu wa Rais la kufanya usafi wa mazingira na kuhakikisha maeneo yote kuwa safi.
ARUSJA DC
KaziIendelee
PICHA ZA MATUKIO WATUMISHI WAKIFANYA USAFI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.