Na. Elinipa Lupembe.
Watumishi wa makao makuu halmashauri ya Arusha, wameendelea kutekeleza agizo la mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, la kufanya usafi katika maeneo ya ofisi zote za serikalia, kila siku ya Alhamisi ya wiki.
Watumishi hao, kwa umoja wao wamefanya usafi katika maeneo yote yanayozunguka ofisi za halmashauri hiyo, wakiwa na mafagio, mafyekeo, majembe na mazoleo taka, huku wakihakikisha maeneo yote yanakuwa safi kwa afya zao.
Hata hivyo watumishi hao, wapongeza hatua hiyo ya kupata walau saa moja ya kufanya usafi kwa wiki, wakithibitisha kuwa usafi wa maeneo ni jukumu la kila mtu anayeishi na kufanyia shughuli eneo husika.Aidha wameitaka jamii kutambua kuwa, kufanya usafi katika maeneo wanayoishi ama maeneo wanayofanyia shughuli zao za kila siku, uwe na duka, genge, ofisi, hoteli n.k, ni jukumu lako kufanya usafi maeneo yanayoku, na sio jukumu la serikali kama watu wanavyodhani.
"Kila mtu anawajibu wa kufanya usafi katika eneo analoishi ama analofanyia shughuli ndani na mazingira ya nje yanayozunguka eneo lake, watu waache kuilalamikia serikali kiwa maeneo ni machafu, bali wafanye usafi kwa afya zao" wamesema watumishi hao.
Awali serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, inawataka wananchi wote kufanya usafi na kuweka mazingira safi kila wakati, ili kuwa na hewa safi na kupambana na magonjwa yanayotokana na uchafu.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.