WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KIZALENDO NA KWA KUJITUMA.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mhe.Amir Mohammed Mkalipa amewataka watumishi wa umma Wilayani Arumeru kufanyakazi kwa moyo wa kizalendo nyakati zote za utumishi wao ili kuwa kielelezo kwa vizazi vijavyo.
Mkalipa amesema hayo wakati wa sherehe mahafali ya 8 ya kidato cha sita ikiwa sambamba na sherehe ya kumuaga rasmi Mkuu wa Shule hiyo Ndg.John Massawe aliyehudumu shuleni hapo Kwa Miaka 21.
Akizungumzia suala la uzalendo,,mhe.Mkalipa amesema kuwa Mwl.Masawe amekuwa kielelezo cha utumishi uliotukuka kwani shule hiyo imekuwa mara kwa mara ikifanya vizuri katika ufaulu wa Kitaifa chini ya usimamizi wa Mkuu huyo wa Shule mstaafu kwani wanafunzi wamekuwa wakipata ufaulu wa madaraja ya juu, huku akimtaka Mkuu wa shule mpya pamoja na wanafunzi kuendeleza juhudi ili kulinda hadhi ya shule hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Bi Nai Molle ameongeza kwa kusema kuwa mkuu huyo wa shule Mwl.John Massawe ni mfano wa kuigwa na Kiongozi wa kipekee ambae amemudu kufanya kazu katika mazingira magumu na ambayo ameweza kuyabadilisha na sasa ni kivutio na shule ya mfano Kitaifa.
Ameongeza kusema kuwa walimu wa shule ya sekondari Mwandet, wanajuhudi kubwa katika kuwafundisha watoto, na matokeo ya juhudi hizo yanaonekana wazi jambo ambalo limetugusa wazazi wote, na kufanya maamuzi ya kumnunulia gari Mkuu wa Shule John Massawe ikiwa ni shukrani kwa kazi nzuri aliyofanya Kwa Miaka 21 ya Utumishi wake.
"Shule ya Mwandeti ni kubwa, ina walimu wengi, haina nyumba za kutosha kuishi walimu wote hapo shuleni, lakini pia eneo hili halina nyumba za kupangisha, hivyo asilimia kubwa ya walimu hulazimika kuishi Ngaramtoni, huku kukiwa hakuna usafiri wa kuaminika kufika shuleni, walimu wanateseka sana, wazazi tumeamua kuwaondolea adha hiyo wakati wakiwahudumia watoto wetu" amesisitiza Mwenyekiti huyo.
Aidha amefafanua kuwa Mkuu wa Shule John Massawe alihamasiaha ununuzi wa gari aina ya coaster ambao, umegharimu kiasi cha shilingi milioni 48, fedha zilizopatikana kwa kila wazazi kuchanga kiasi cha shilingi elfu thelathini, jambo ambalo limefanyika kwa muda wa miezi miwili baada ya makubaliano ya kikao cha wazazi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.