Na Elinipa Lupembe
Wauguzi halmasahuri ya Arusha, wametakiwa, kutoa huduma rafiki kwa wagonjwa kwa kufanya hivyo kutawafanya wagonjwa kujisikia wanapata ahueni kabla ya hata ya kupatiwa matibabu na dawa.
Rai hiyo imetolwa na Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, wakati akifungua semina ya Wauguzi wa halmasahuri hiyo, ya kukumbushana namna ya utekelezaji wa majukumu yao na misingi na maadili ya taaluma ya uuguzi.
Mkurugenzi Msumi, amefafanua kuwa taaluma ya uuguzi ni wito ambao unamlazimu muuguzi kujitoa kabla ya kuweka maslahi mbele kwa kutumia lugha nzuri kwa mteja wake, ili kumfanya mgonjwa ajisikie yuko kwenye mikono sahihi tayari kwa kupata uponyaji.
"Mtu anapokuwa mgonjwa kwanza hayuko sawa kiakili, kimwili na kisaikolojia, huduma ya kwanza anayotakiwa kupewa ni faraja na upendo, kwa kufanya hivi mgonjwa anaanza kupona kabla hata ya kupata matibabu yenyewe, mkishindwa kufanya hivyo, malalamiko yote ya wagonjwa yanakuja kwa serikali, fanyeni kazi kwa uadilifu ili kufikia malengo ya serikali" Amesisitiza Msumi
Aidha amewakumbusha wauguzi hao kuwa Serikali imewaamini na kuwapa jukumu la kuwahudumia watanzania ambao ni wagonjwa, ni vema kila mtu akatimiza majukumu yake huku akiweka mbele uzalendo, utayari, utii, uwazi na uwajibikaji, ili kufikia lengo la serikali la kutoa huduma bora kwa jamii.
Hata hivyo wauguzi hao, wamefurahishwa na semina hiyo, ambayo wamekiri imewapa fursa ya kubadilisha uzoefu wa namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wauguzi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuipongeza serikali ya mama Samia kwa kuendelea kuboresha miundominu ya Afya pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, jambo ambalo linawapa moyo na ari ya kufanya kazi na kuwahudumia wagonjwa kwa bidii.
Nmnyaki Lazaro muuguzi kituo cha afya Nduruma amesema kuwa, wao kama wauguzi, wana jukumu kubwa la kuwahudumia wagonjwa kwa kuzingatia uwajibikaji wenye tija na kutoa huduma bora na rafiki kwa wagonjwa bila kujali changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.
Modeta Patrick, muuguzi zahanati ya Ngorbon amethibitisha kuwa kupitia mafunzo hayo, wamejipanga kutoa huduma bora inayozingatia misingi na maadili ya taaluma ya uuguzi hususani katika eneo la huduma bora kwa mteja.
Naye Muuguzi Mkuu, halmashari ya Arusha Neomi Temu, amesema kuwa, lengo la semina hiyo ni, kuwakumbusha wauguzi hao namna bora ya utekelezaji wa majukumu yao hususani katika kipengele cha huduma bora kwa mteja, huduma ambayo ikitolewa kwa ufasaha, inaleta faraja kubwa kwa wagonjwa na kuendelea kuiamini taaluma ya uuguzi.
Inafahamika kuwa asilimia 80 ya wahudumu katika sekta ya afya ni Wauguzi, hivyo wakiwekewa mazingira rafiki ya kutoa huduma kwa wagonjwa, na wao kujituma na kufuata misingi na maadili ya kazi yao, iitapunguza malalamiko na kuongeza ufanisi katika fani ya utabibu nchini.
ARUSHA DC
KaziInaendelea
JIANDAE KUHESABIWA
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MAFUNZO YA WAUGUZI
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akifungua semina ya Wauguzi iliyofanyika katika ukumbi wa halmasahuri ya Arusha
Mganga mkuu wa halmashauri ya Arusha, Dkt. Petro Mboya akiongea na wauguzi wa halmashauri ya Arusha
Wauguzi wakiwa katika semina ya Wauguzi ya kukumbushana namna ya utekelezaji wa majukumu yao na misingi
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.