Na Elinipa Lupembe
Wakazi wa halmashauri ya Arusha wameipongeza serikali ya awamu ya sita, kwa kurahisisha upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa chini ya miaka mitano, kwa kusogezewa huduma hiyo karibu, jambo ambalo limewezesha watoto kupata vyeti vya kuzaliwa kwa sasa tofauti na hapo awali.
Upendo Mathayo (27) mama wa watoto watatu, mkazi wa Kisongo, amethibitisha kupata cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake wa mwisho aliyemtaja kwa jina la Isack Elias mwenye mwezi mmoja sasa, na kuongeza kuwa utaratibu huo ni mzuri umewarahisishia watoto wao kupata vyeti hivyo, vyeti ambavyo hata yeye na watoto wake wake wakubwa mpaka leo hawajavipata.
Nilijifungua mtoto wangu kwenye kituo cha Kivulini ' Martenity Africa' na kusajiliwa baada ya wiki moja nilirudi na kupatiwa cheti cha mtoto cha kuzaliwa, mtoto wangu ana mwezi mmoja lakini ameshapata cheti, sikuamini kwa kuwa mika ya nilitafuta cheti changu cha kuaziliwa sikukipata". Amesema Upendo
Neema Emanuel (29) mkazi wa Oldonyosapuk, amethibitisha kupata cheti cha kuzaliwa cha mtoto Jovine Timoth (6) kupitia ofisi ya Mtendaji wa kata wakati wa kampeni ya mwaka uliopita, na kuipongeza serikali kwa utaratibu huo mzuri na rahisi unawawezesha hata watu wanaoishi vijiji kuoata huduma hiyo ndani ya maeneo yao wanayoishi.
Naye Afisa Utawi wa Jamii, halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi amethibitisha urahisi wa upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa huku jumla ya watoto 51,751 katika halmashauri hiyo sawa na 85.4 % wamesajiliwa na kupatiwa vyeti, kutoka makisio ya watoto 58,549 waliotarajiwa kuandikishwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022, zoezi ambalo linafanyika kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya pamoja na ofisi za kata.
Afisa Utawi huyo amefafanua kuwa, baada ya RITA kugatua madaraka kwa vituo vya afya, kumekuwa na urahisi wa upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa huku wazazi na walezi wakiwa na muitikio chanya wa kusajili watoto ili wapate vyeti vya kutokana na Serikali kurahisisha taratibu za usajili kwa kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi.
"Kwa sasa serikali imewarahisishia wazazi na walezi, kusajili na kuchukua vyeti vya watoto wao, huduma hii inapatikana kwenye vituo vya afya, mara baada ya mama kujifungua, humsajili mtoto kupitia kadi yake ya kliniki na kupata cheti cha kuzaliwa kwa wakati" Amefafanua Beatrice
Serikali kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) iligatua madaraka kwa halmashauri kupitia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na ofisi za kata lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa Tanzania anapata cheti cha kuzaliwa kwenye kituo cha afya alichozaliwa kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano.
ARUSHA DC
TUPO KAZINI✍✍
Muuguzi Mfawidhi hospitali ya Wilaya ya Olturumet Dorice Kahwa akimsajili mtoto kwa ajili ya kupata cheti cha kuzaliwa mara baada ya mama huyo kujifungua hospitalini hapo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.