Na Elinipa Lupembe
Wazazi na walimu wametakiwa kutumia muda wa makuzi ya watoto, kuwafundisha kupenda miti ili kuwajengea tabia ya kutunza mazingira, urithi ambao na wa thamani kubwa kwa maisha ya wanadamu na viumbe vyake.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mhe. Ojung'u Salekwa, wakati akiwashukuru wananchi wa kijiji cha Shiboro kata ya Sambasha waliojitokeza kupanda miti kwenye eneo la shule mpya ya msingi Shiboro.
Mwenyekiti Ojung'u, ametumia nafasi hiyo, kuzungumza na wanafunzi, na kuwasisitiza kila mmoja kupanda mti nyumbani na shuleni na kuinadika majina yao, alama ambayo haitafutika maishani mwao.
"Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, wazazi na walimu tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha tunawafundisha watoto wetu tabia ya kupenda miti kwa kupanda na kuitunza, jambo ambalo ni urithi wenye thamani kubwa katika maisha yao na vizazi vijavyo". Amesisitiza Mwenyekiti Ojung'u
Aidha amesistiza kuwa, serikali imetekeleza jukumu lake la kuwaletea miti, kazi kubwa iliyobaki kwa wananchi ni kuitunza na kuhakikisha miti yote inakuwa kwa idadi yake na kuwashauri kuweka vibao kwenye maeneo ya Umma vya kuzuia mifugo kuingia, pamoja na kutoza faini pindi mfugo utakapokula mti.
Hata hivyo Diwani wa Kata ya Sambasha Mhe. Mosses ameahidi kushirikiana na viongozi wa vijiji, kusimamia ukuaji wa miti hiyo na kuhakikisha miti yote inakuwa kama ilivyopandwa kwa kuwa hali ya hewa ni rafiki kwa miti.
"Nakuahidi mwenyekiti, miti yote itakuwa kama ilivyopandwa, miti ilikuwa ni hitaji letu kubwa, tumejipanga na serikali za vijiji kusimamia na kutoa taarifa ya upandaji miti kila kikao cha robo ya mwaka". Amesema Mhe. Diwani
Lea Alex mwanafunzi wa darasa la 6 shule ya Msingi Timbolo, amekiri kupenda miti kutokana na faida zake ambazo amefundishwa darasani pamoja na hamasa zinazotolewa na Serikali na wadau wa mazingira.
"Nitapanda miti, shuleni na nyumbani pamoja na kuitunza ili ikie". Amesema Lina
Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, KaziIendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.