• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAZAZI NCHINI WATAKIWA KUSIMAMIA WATOTO, MATUMIZI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI.

Posted on: June 15th, 2020

Na Elinipa Lupembe.

     Wazazi na walezi wametakiwa kuwasimamia watoto wao, katika matumizi ya vifaa vya kielekroniki ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ngono na ukatili mwingine kupitia taarifa zilizopo mitandaoni.

       Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu, Jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishiwa tarehe 16, Juni  kila mwaka.

        Waziri Ummy amesema, kuwa katikanyakati hizi, tumeshuhudia watoto wanatumia vifaa ya kielektroniki, ikiwa pamoja na simu na kompyuta kwa lengo la kujifunzia mambo ya masomo, hivyo ni vyema wazazi kuwasimamia watoto wao katika mayumizi ya vifaa hivyo, na kuhakikisha wanazingatia matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kuepusha kuanza kuiga na kufanya vitendo vya kikatili.

       Amewasisitiza  Wazazi na Walezi kuhakikisha, Usalama wa watoto wakati wote wakiwa nyumbani, katika kipindi hiki pamoja nakuwazuia kwenda kwenye maeneo hatarisgi kwa usalama wao kwa kufanyiwa vitendo vya ukayili, ikiwa ni pamoja na kubakwa, kulawitiwa, kushawishiwa kufanya ngono na hata kupata maambukizi ya Corona.

    “Katika eneo la malezi ya watoto wetu bado tuna changamoto kubwa ya matumizi ya mitandao, wazazi na walezi tuhakikishe tunawasimamia watoto wetu wasijiingize katika masuala yasiyofaa katika mitandao hiyo” alisema Waziri huyo.

    Aidha Waziri Ummy amaesema kumekuwa na ongezeko la matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini, kutokana na ukweli kuwa, wananchi wengi wamepata uelewa na kuweza kutoa taarifa katika maeneo maalum yaliyoainishwa na  Serikali.

    Hata hivyo Waziri Ummy, ameweka wazi  takwimu za mikoa ya kipolisi iliyoongoza kuwa na matukio mengi zaidi ya ukatili dhidi ya watoto kwa mwaka 2018 ni  Mkoa wa Tanga (1,039), Mbeya (1,001), Mwanza (809) na Arusha (792) na kwa mwaka 2019 ni Mkoa wa Tanga (matukio 1,156), Mkoa wa Kipolisi-Temeke (844), Mbeya (791) na Mwanza (758).

      Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sebastian Kitiku, amewasisitiza wazazi kuwajibika katika malezi kwa kuhakikisha wanawasimamia watoto wao kwa kufuatilia kwa karibu masuala ambayo yanaweza kusababisha ukatili kwa watoto.

     “Wazazi tuwaangalie watoto wetu tusiwaache watoto wakajiamulia baadhi ya vitu ambavyo vitawasababisha waingie katika mambo ambayo yatapelekea kufanyiwa vitendo vya kikatili” alisema Kitiku.

     Maadhimisho ya  Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2020  yenye Kauli mbiu ya  “Mifumo Rafiki ya Upatikanaji Haki ya Mtoto: Msingi Imara wa Kulinda Haki Zao”


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.