Na Elinipa Lupembe
Wazazi wametakiwa kutenga muda wa malezi kwa watoto nakuhakikisha wanaongea nao masuala mablimbali ya makuzi ili kufahamu mahitaji yao ya kihisia, maoni yao na changamoto zinazowakabili lengo likiwa ni kupunguza matukio ya kikatili dhidi yao, matukio ambayo yameathiri watoto wengi kiakili na kisaikolojia.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi wakati wa uzinduzi wa mradi wa .............. ...... awamu ya pili, mradi unaotekelezwa na shirika la Center for Women and Children Development.
Msumi amesema kuwa wanaweza kuepuka kufanyiwa matendo ya kikatili kama watajitambua wao wenyewe kwanza, na mtu wa kwanza kuwafanya wajitabue ni wazazi, hivyo ni jukumu la wazazi kutenga muda wa kuwa karibu na watoto wakati wote wa ukuaji wao, licha ya changamoto za kujitafutia pato la familia.
“Kwa sasa wazazi /walezi na jamii, wameanza kushtushwa na ongezeko la matukio ya ukatili dhidi ya watoto sambamba na kufahamu athari zake, na kuanza kushirikiana kukabilianana nayo, hivyo tuendele kujipanga hasa kwa kuwa na muda kwa ajili ya malezi licha ya majukumu mengi ya kikazi yanayowakabilia”. Amesema Mkurugenzi Msumi.
Aidha amewataka wazazi kuwa makini na ndugu jamaa na marafiki, wanaoishi na wale wanaowatembelea nyumba, wamekuwa ni chanzo cha watoto kujifunza tabia mbaya pamoja na kuwafanyia vitendo viouvu hususani ubakaji na ulawiti.
"Matukio mengi ya ukatili kwa watoto yanayotokea kwenye jamii yanafanywa na ndugu, jamaa, marafiki nawatu wa karibu na familia na jamii, jambo ambalo linaathiri hata mwenendo wa kesi za watoto mahakami kushindwa kutoa ushahidi kwa kuhofia kuharibu uhusino wa familia, kabla ya kutokea hayo ni vema kuwa makini na watu hao, zaidi watoto watabaki salama" Amesema Msumi
Naye Mwenyekiti wa Halamsahuri ya Arusha Mhe. Dkt. Ojung’u Salekwa ameweka wazi kuwa uongozi wa halamshauri kupitia waheshimiwa madiwani wako tayari kupambana na masuala ya ukatili kwa kuendelea kutoa elimu kwenye jamii zao licha ya changamoto za ukinzani wa mil ana desturi zao.
Ameongeza kuwa, wao kama viongozi wa wananchi wanahamasisha jamii na kuhakikisha kila mwanajamii anahusika kupinga ukatili dhidi ya watoto, mapenzi ya jinsia moja ambayo ni wimbi kubwa pamoja na kuwafuatilia watoto wao dhoidi ya matu,mizi ya mitandao ya simu na matumizi sahhi ya televisheni nyumbani.
“Watoto wanajifunza mambo mengi kutoka kwa wazazi na jamii, wazazi hakikisheni mnadumisha amani nyumbani ili watoto waweze kujifunza matendo yaliyo mema, lugha zisizo na staha kama vile matusi ni moja ya chanzo cha kuwakuza watoto wakiwa na makuzi mabaya” Amesisitiza Mwenyekiti huyo
Hata hivyo Mkurugenzi wa Shirika la CWCD Hindu Mbwegu, amesema kuwa kama wazazi na walezi watasimama kwenye sehemu ya watoto watakuwa salama dhidi ya matukio mengi ya kikatili yanayoathiri watoto katika ukuaji wao.
Ufuatiliaji wa maendeleo ya mtoto shuleni, ikiwemo kuchunguza marafiki wa mtoto awapo shuleni ili wasimuambukize mtoto tabia isiyo na maadili kwa hiyo inaweza kuwa mojawapo ya sababu za ukatili kwa watoto na kuongeza kuwa Taifa linategemea kizazi cha leo ili waweze kuwa viongozi, Hivyo ni lazima kuwekeza malezi bora kwa watoto hao kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
Mradi wa …..unatekelezwa kwenye kata 6 za Olturoto, Naurei, llboru, Kiranyi, Olturumet na Moivo kwa ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Scociety kuanzia mwezi Juni mpaka Novemba 2023 kwa kuwezesha maabara 6 za watoto wakiume, kuwawezesha wabab wa zamu kutembelea maambara z watoto.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.