• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI JAFO AWATAKA WANANCHI WA ARUSHA KUPANDA MITI, ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Posted on: January 18th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Dr. Seleman Jafo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha, kuelekeza nguvu katika kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, yanayosababisha ukame na ongezeko la joto duniani hususani katika maeneo mengi ya Tanzania kwa sasa.

Waziri Jafo ametoa rai hiyo, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua vyanzo vya maji vya Usa -River na Midawe  katika wilaya ya Arumeru na kusema kuwa, kwa sasa matokeo hasi ya mabadiliko ya tabia nchi, yamejitokeza dhahiri huku yakileta madhara kwa jamii na mali zao.

"Ukiangalia hali ya hewa nchini imebadilika sana, joto limeongezeka kwa kasi, mfano hali ya hewa ya Arusha ilikuwa ni baridi sana, ila sasa kuna joto, joto ambalo limesababisha ukame katika maeneo mengi, ukame ambao umeanza kuleta madhara kwa watu na mali zao, ikiwemo vifo vya mifugo, jambo ambalo tunapaswa kuchukua hatua za haraka kwa kuweka mikakati thabiti ya kutunza mazingira yetu" Amesisitiza Mheshimiwa Waziri Jafo.

Licha ya Waziri Jafo, kuridhishwa na hali ya utunzaji wa mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji, wilayani Arumeru, amesisitiza kuendelea kutunza vyanzo hivyo vya maji pamoja na kuwa na mikakati endelevu kwa kupanda miti, ikiwa ni pamoja na halmashauri kuwezesha kila mwanafunzi kuotesha mti mmoja katika shule na maeneo yanayozunguka shule zao.

Hata hivyo Waziri Jafo amezitaka halmashauri kuhakikisha zinaweka bajeti ya utunzaji na uendelezaji wa mazingira asilia, hasa kwa kuwekeza kwenye  uanzishwaji wa vitalu vya miti, kuhamasisha jamii kuotesha miti kwa wingi katika maeneo yao, jambo litakalorudisha ikolojia ya mazingira, inayoanza kuharibika kwa sasa.

Aidha katika ziara hiyo, mheshimiwa Jafo amefanikiwa kuotesha miti kwa kushirikiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Bangata halmashauri ya Arusha, katika eneo la tanki la maji Midawe linalomilikiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha 'AUWSA' na kugawa miti kwa wanafunzi wa shule hiyo, kwa ajili ya kuiotesha  kuzunguka eneo hilo la chanzo cha maji, chanzo kinacholisha maji kwa wananchi wa eneo la Arumeru na Jiji la Arusha.

Afisa Mazingira Bonde la Mto Pangani, Felista Joseph, amethibitihsa kupungua kwa kiasi cha maji kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu na baadhi ya watu kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji, lakini Bonde la mto Pangani linasimamia vyanzo vya maji nchini huku likiwa na jukumu la kugawa matumizi ya maji kukingana na kiasi cha maji ili yaweze kutosheleza kwa watumiaji wote bila kuleta migogoro katika jamii.

"Kiasi cha maji kilichopo kinagawanywa kwa makundi kulingana na matumizi, wapo watumiaji wa kubwa ambao ni Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira nchini na makampuni yanayomiliki mashamba makubwa, watumiaji wadogo wa mifereji na kubakiza kiasi cha maji kwa ajili ya mazingira na viumbe vyake" amefafanua Afisa Mazingira wa Bonde la Mto Pangani.

Naye Mkuu wa wilaya ya Aruemeru, Mhandisi Richard Ruyango, licha ya kumshukuru Mheshimiwa Waziri huyo, kwa kutembelea na kukagua hali ya utunzaji wa mazingira katika wilaya ya Arumeru, ameahidi kutekeleza maagizo na ushauri uliotolewa na Waziri huyo, kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anapanda mti mmoja pamoja na kuongeza bajeti ya mazingira katika halmashauri zote za Arusha na Meru, huku wakiweka kipaumbele katika kuhamasisha jamii kwenye utunzaji wa mazingira hasa wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji.

Katika ziara hiyo ya siku moja, Waziri Jafo ametembelea chanzo cha maji USA River,  bustani ya Miti halmashauri ya Meru na chanzo cha maji na Kituo cha maji cha AUWSA kilichopo Midawe, halmashauri ya Arusha.













Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.