Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo ameshauri kujengwa jengo jipya la upasuaji katika kituo cha Afya Nduruma na kuamurujengo la upasuaji lililopo kutumika kwa kazi nyingine kutokana na jengo hilo kuwa dogo kulingana na matarajio ya huduma inayotegemewa kutolewa katika kituo hicho.
Waziri Jafo amesema hayo wakati wa kuweka Jiwe la Msingi katika kituo cha hicho cha Afya halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua ujenzi na upanuzi wa miundo mbinu unaoendelea kituoni hapo.
Licha ya Waziri Jafo kushauri kuanza ujenzi wa jengo jipya la upasuaji na kuacha la zamani lakini pia amekiri kuridhishwa na ujenzi huo wa miundo mbinu yote unaoendelea na kuongeza kuwa huo ni utekelezaji wa agenda kuu ya serikali ya awamu tano ya kuboresha sekta ya Afya.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.