WAZIRI KOMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA TAASISI YA ‘THE GATES’
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Afrika wa ‘The Gates Foundation’, Dkt. Paulin Basinga aliyemtembelea tarehe 3 Februari 2025 katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo ya viongozi hao yaliangazia maboresho yaliyofanyika katika sekta ya Afya nchini Tanzania hususan afya ya Mama na Mtoto.
Pia, wamejadili juu ya Tuzo ya ‘Goalkeepers’ ambayo atapokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla itakayofanyika tarehe 4 Februari 2025, jijini Dar es Salaam.
‘Goalkeepers Awards’ hutolewa kwa viongozi wa kimataifa na watu mashuhuri kama sehemu ya kutambua mchango wao katika maendeleo ya jamii ili kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa.
Mheshimiwa Rais Samia ni miongoni mwa vinara wa Maendeleo waliotambuliwa na taasisi hiyo kufuatia maboresho na mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini Tanzania katika huduma za afya ya mama na mtoto.
Taasisi ya ‘the Gate’ ilizinduliwa mwaka 2000 kwa lengo la kuboresha programu za afya duniani na kupunguza umasikini uliokithiri kupitia maeneo makuu matatu ya msaada ambayo ni Mfuko wa Maendeleo ya Dunia, Mfuko wa Afya ya Dunia na Programu za Marekani.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.