WAZIRI MKUU AWASILI MKOANI ARUSHA, KUMUWAKILISHA RAIS MARIDHIANO DAY.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Februari 26, 2025 amewasili Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Christian Makonda. Mhe. Majaliwa yupo Mkoani Arusha akitarajiwa kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya siku ya maridhiano, maadhimisho yanayotarajiwa kufanyika Februari 27, 2025 kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano Jijini Arusha AICC.
Jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania ilianzishwa March tatu mwaka 2016 kwa lengo la kudumisha amani Tanzania.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.