WAZIRI NDUMBARO AKUTANA NA RC MAKONDA, KUONGEZA ARI KAMPENI YA MAMA SAMIA ARUSHA.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumatatu Machi 03, 2025, amekutana na kufanya mafungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro Ofisini kwake Jijini Arusha.
Waziri Ndumbaro yupo Mkoani Arusha kukagua utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, kampeni ambayo imezinduliwa Machi 1,2025 ikiambatanishwa na Wiki ya wanawake ambayo kilele chake kinafanyika Machi 08, 2025 na Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kampeni ya Mama Samia kwa Mkoa wa Arusha inafanyika kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid huku Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda akitoa wito kwa wananchi wote wa Arusha wenye changamoto mbalimbali za kisheria kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo iliyoasisiwa na kufadhiliwa na Rais Samia katika jitihada zake za kupunguza migogoro kwa kijamii kote nchini na kutoa msaada wa kisheria na Mawakili kwa wasiokuwa na uwezo na wale wa pembezoni wasiofikiwa kwa karibu na huduma za sheria.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.