Na Elinipa Lupembe
Mfanyabiashara Wilfred Daniel amechakuguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Wafanya biashara wilaya ya Arumeru baada ya kushinda kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmasahuri ya Meru, Baraza linalojumuisha halmashauri za Arusha na Meru zinazounda wilaya ya Arumeru.
Mfanya biashara huyo amepata nafasi hiyo, na kupewa dhamana ya kuliongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka 3, kwa kupata kura 19 kati ya kura 49 zilizopigwa na kuwashinda wagombea wenzake watatu waliowania nafasi hiyo.
Awali Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara wilaya ya Arumeru ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, kwa mujibu wa Kanuni, amemtangaza Mfanyabiashara Wilfred Daniel kuwa Mwenyekiti mwenza wa Baraza hilo, huku akimtangaza Makamu Mwenyekiti Mwenza CPA. Maija Mchau aliyepata kura 17.
Aidha Mhandisi Ruyango, amewataka viongozi hao kusimamia miongozo na kuyafahamu madhumuni ya Baraza ili kuweka mkakati wa utekelezaji na kuyafikia malengo ya baraza kwa kushirikishana kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara kwa maendeleo ya wananchi na Taifa.
"Serikali inatambua huduma mnayoitoa kwa jamii, ninawaagiza viongozi, kaeni na wafanyabiashara wenzenu mpate maoni yao, ili kuishauri serikali namna bora ya kuenenda ili kuwa na mazingira rafiki ya kuendesha biashara, yanayochochea maendeleo binafsi na ya Taifa". Amesisitiza mkuu huyo wa wilaya
Hata hivyo baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti mwenza licha ya kuwashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo , ameahidi kushirikiana na wafanyabiashara wote kwa kuitumikia nafasi hiyo kwa uaminifu ili kufikia lengo la serikali kupitia Baraza la wafanayabishara la kuwaunganisha na serikali.
Mkuu wa Idara ya Biashara na Uwekezaji, halmashauri ya Meru, Noel Pallangyo ameyataja madhumuni ya Baraza la Biashara la wilaya ni kuwakutanisha Sekta Binafsi na Serikali ili kujadili na kupeana ushauri wa namna ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika Wilaya na kukuza sekata ya uchumi.
Majukumu mengine ni pamoja na kutengeneza mazingira bora ya kufanyia Biashara na uwekezaji, Kuibua fursa za uwekezaji, kuzinadi fursa hizo kupitia makongano mbalimbali pamoja na kufanya matangazo ya biashara.
Baraza la Taifa la Biashara la wilaya lilianzishwa chini mwaka 2001 kwa waraka wa Rais na 1 wa mwaka 2001 ukielekeza kila wilaya liunde Baraza la Biashara la Wilaya ikiwa ni jitihada ya kukuza uchumi ndaninya wilaya, wilaya ya Arumeru imeunda Baraza hilo na kuchagua viongozi watakaoongoza kwa miaka miatatu.
Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Biashara wilaya ya Arumeru, Wilfred Daniel, akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo mara baada ya kutangazwa mshindi na kushika nafasi hiyo kwa miaka mitatu.
Makamu Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Biashara wilaya ya Arumeru, CPA. Maija Mchau akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kwa miaka mitatu.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, akiongoza mkutano wa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2022/2023, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Meru
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa Baraza la Biashara wilaya ya Arumeru uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Meru
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa Baraza la Biashara wilaya ya Arumeru uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Meru
Wakuu wa Idara na Vitengo, halmashauri ya Arusha wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la Biashara wilaya ya Arumeru uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Meru
Wakuu wa Idara na Vitengo, halmashauri ya Arusha wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la Biashara wilaya ya Arumeru uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Meru
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.