#Watoto ni rasilimali muhimu sana inayoweza kufananishwa na madini ya dhahabu au petroli, ni jukumu la taifa kuiandaa vyema raslimali hiyo muhimu kwa uhai wa Taifa endelevu.
#Taifa lenye misingi imara, huwekeza kwa watoto kwa kuwatunza, kuwajali na kuwaendeleza kwa kupiga vita kwa vitendo, ukatili dhidi yao.
#Ni jukumu letu sote kuwapa watoto haki zao za msingi, na kutambua kuwa, kuwapa watoto haki zao sio hisani wala upendeleo bali ni majukumu ya lazima kwa wazazi,walezi na jamii kwa ujumla.
#Halmashauri imeunda mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya kata na halmashauri, kwa lengo la kuhakikisha watoto wanakutana na na kujadili changamoto zinazowakabili na kuzitolea taarifa, ikiwa ni pamoja na kupaza za kupiga vita ukatili dhidi yao.
#Halmashauri pia inatumia Timu ya wanawake, MTAKUA, kuwezesha malezi na usimamizi imara kwa watoto ili kuwaanda kuwa na taifa imara kuelekea uchumi wa viwanda.
#Halmashauri inashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, wanaojihusisha na masuala ya watoto kwa kuwajengea watoto uwezo na kuwapa maarifa juu ya haki, ulinzi na usalama wao na jinsi ya kujikinga dhidi ya ukatili, unaendelea kwenye jamii yao.
#Kuhamasisha jamii hususani wanawake katika uanzishaji wa Viwanda vidogo na vya kati ili waweze kujiinua kiuchumi na kuwasaidia watoto kupata mahitaji yao ya msingi.
#Mtoto ni Msingi wa Taifa Endekevu, Tumtunze, Tumlinde na Kumuendeleza#
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.