Na. Elinipa Lupembe.
# Wananchi wa kata ya Musa bado wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, lakini tayari halmashauri imeshasaini mkataba na Mkandarasi wa kampuni ya Winning Spirit Construction, kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi wa maji Likamba kwa awamu ya pili kwa gharama ya shilingi bilion 1.8, moja ya mradi wa maji wa vijiji kumi ya mwaka 2012, mradi huo ukikamilika utahusisha kijiji cha Likamba na vitongoji vyake.
# Wananchi wote wametakiwa kuwatunza mbwa wao, ikiwemo kuwapa chakula na kuwafungia, pamoja na kuwapatia chanjo hasa za kichaa cha mbwa, pamoja na kuwa na mkakati wa kupunguza idadi ya mbwa wafugwao, ili kupunguza idadi kubwa ya mbwa wanaozurura.
# Wamepongeza juhudi na mafanikio ya halmashauri kwa kusajili shule mbili mpya za sekondari kwa kipindi cha robo ya pili, ikiwa ni shule ya sekondari Losikito kwa usajili namba S. 5110, na shule ya Sekondari Oldonyowas kwa namba S. 5111. Huku jumla ya wanafunzi 327 walipangiwa kuanza kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2019, mpaka sasa jumla ya wanafunzi 283, wameripoti na wameshanza masomo yao katika shule hizo.
#Mafisa Watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha mikutano ya kisheria ya vijiji, inafanyika kila robo ya mwaka, yaani kila baada ya miezi mitatu, endapo Mwenyekiti wa kijiji hataitisha mikutano hiyo mara tatu mfululuzizo, sheria inaruhusu kumuondoa kwenye nafasi yake, utaratibu ufanyike kwa ajili ya kuwaondoa wenyeviti wa vijiji wasioitisha mikutano ya kisheria katika vijiji vyao.
# Madiwani wameiomba Serikali kuunga mkono, juhudi za wananchi ambao wannanzisha Miradi ya maendeleo katika maeneo yao, kwa kuongezea kiasi cha fedha ili kukamilisha miradi hiyo, hali ambayo itawatia moyo wananchi hao kuendelea kuchangia miradi katika maeneo yao.
# Kumekuwa na changamoto ya baadhi ya vijiji kutokufikiwa na umeme wa REA huku baadhi ya maeneo yakiishia kuwekwa nguzo, hivyo Wameutaka uongozi wa Mpango wa umeme vijiji - REA kualikwa kuhudhuria kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la tarehe 18.02.2019 ili kuweza kutoa ufafanuzi juu ya changamoto hiyo kwa wawakilishi hao wa wananchi.
#Wamekubaliana madiwani kuendelea kushirikiana na wananchi pamoja na watalamu wa ngazi ya kata na halmashauri, kutatua baadhi y a changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wao, changamoto nyingi zinawezekana kutatulika ndani ya maeneo yao.
# Wazazi wametakiwa kuona umuhimu wa watoto kupata chakula cha mchana wawapo shuleni na kuwataka kushiriki kuchangia upatikanaji wa chakula bila kuona suala hilo ni adhabu bali ni jukumu lao.
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI
Makamu Mwenyekiti, halmashauri ya Arusha na Diwani wa kata ya Oloirien, Mhe. Albert Oltereu akiwasilisha taarifa za kata ya Oloirien
Diwani wa kata ya Olmotony, Mhe. John Slim akiwasilisha taarifa za kata ya Olmotony.
Diwani wa kata ya Mateves Mhe. Juliu Mollel akiwasilisha taarifa za kata ya Mateves.
Diwani wa kata ya Olkokola Mhe. Kalanga Laiza akiwasilisha taarifa za kata ya Olkokola.
Diwani wa kata ya Musa, Mhe. Florah Zelote akiwasilisha taarifa za kata ya Musa.
Diwani wa kata ya Ilkiding'a Mhe. Loth Mungaya akiwasilisha taarifa za kata ya Ilkiding'a.
Diwani viti Maalum, Mhe. Nuru Ndosi akiwasilisha taarifa za kata ya Kiranyi.
Diwani wa kata ya Nduruma, Mhe. Raymond Mollel akiwasilisha taarifa za kata ya Nduruma.
Diwani wa kata ya Olturoto, mhe. Baraka Simon akiwasilisha taarifa za kata ya Olturoto.
Diwani wa kata ya Kimnyaki, Mhe. Olais Wavii akiwasilisha taarifa za kata ya Kimnyaki.
Diwani wa kata ya Tarakwa, Mhe. Elihuruma Laizer akiwasilisha taarifa za kata ya Tarakwa.
Diwani Viti Maalum, Mhe. Happiness Laizer akiwasili taarifa za kata ya Bangata.
Diwani wa kata ya Kiutu, mhe. Zephania Sirikwa akiwasilisha taarifa za kata ya Kiutu.
Diwani wa kata ya Lemanyata, Mhe. Losieku Kilusu akiwasilisha taarifa za kata ya Lemanyata.
Diwani wa kata ya Oldonyowas mhe. Elisante Nassari akiwasilisha taarifa za kata ya Oldonyowas.
Diwani wa kata ya Oljoro, mhe. Sanari Mepalari akiwasilisha taarifa ya kata ya Oljoro.
Diwani wa kata ya Laroi, Mhe. Ojung Salekwa akiwasilisha taarifa ya kata ya Laroi
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakifuatilia mijalada kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa kuwasilisha taarifa za kata kwa kipindi cha mwezi Oktoba mpaka Disemba 2018.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.