# Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imepokea wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 baada ya kuidhinishwa, kiasi cha shilingi Bilioni 45.4 na Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania katika Mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha mrejesho 2018/19 .
# Idara ya Ardhi iweke vibao kwenye maeneo yote ya mipaka ya halmashauri ya wilaya ya Arusha na halmashauri nyingine, kwa kuanza na maeneo yenye migogoro kwanza.
# Watumishi wote wanaoishi nyumba 519 wapewe masharti na taratibu za kuishi katika nyumba hizo ikiwemo jukumu la kutunza nyumba pamoja na taratibu za kuamua kufanya ukarabati katika nyumba hizo.
# Baraza limekubaliana kubadilisha matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 150 kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa OPD kwenye hospitali ya wilaya ya Olturumet na kuoneka fedha hizo azitoshi kukamilisha jengo hilo la ghorofa, fedha hizo, zitumike kujenga jengo la mama na mtoto katika hospitali hiyo ambalo litakamilika kwa kiasi hicho cha fedha. Hivyo mchakato wa kubadilisha matumizi ya fedha hizo uanze ili fedha mara moja.
# Meneja wa TARURA kubainisha mtandao wa barabara zote, zinazohudumiwa na TARURA na zile zinazohudumiwa na Halmashauri.
# Diwani wa kata ya Oloirien mhe. Albart Oltetelu amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani kwa kipindi cha mwaka mmoja 2018/19.
# Watumishi wote wanaoishi nyumba 519 wapewe masharti na taratibu za kuishi katika nyumba hizo ikiwemo jukumu la kutunza nyumba pamoja na taratibu za kuamua kufanya ukarabati katika nyumba hizo.
Picha za matukio ya mkutano wa Baraza la Madiwani.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.