• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

YALIYOJIRI WAKATI, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIZINDUA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII TASAF*

Posted on: February 18th, 2020

*YALIYOJIRI LEO FEBRUARI 17, 2020 WAKATI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIZINDUA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU   YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII TASAF*

*Aliyoyasema Rais Dkt. Magufuli*

#Kutokana na jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanyika, hali ya umaskini nchini inazidi kupungua. Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti ya Benki ya Dunia ya Septemba, 2019 imeitaja Tanzania kuongoza kwa kasi ya kupambana na umaskini kati ya nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara.

#Nawapongeza viongozi wote waliohusika katika kutekeleza mpango huu, watendaji wa Serikali zote mbili pamoja na wafadhili wote tunaoshirikiana nao kwani matokeo ya mpango huo yameweza kupunguza umaskini katika jamii.

#Kupitia zoezi la uhakiki wa Kaya maskini lililofanyika Novemba 2015 hadi Juni, 2017 limebaini uwepo wa Kaya hewa 73,561, hii ni changamoto kubwa,Naagiza  tatizo hili lidhibitiwe.

#Jumla ya 67% ya kiasi cha fedha kilikua kikielekezwa kwenye kutoa ruzuku, awamu hii ambayo itatumia sh.Trilioni 2.032 tumeboresha kwa kupunguza kiasi cha ruzuku kufikia 38% na 60% ya fedha hizo ambayo ni sawa na sh. Trilioni 1.22 itatumika kwenye miradi ya maendeleo.

#Awamu hii itatekelezwa katika Halmashauri 185 za Tanzania Bara na Wilaya 11 za Zanzibar. Miradi itakayotekelezwa itahusu sekta za afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara na mazingira, Pia kupitia miradi hiyo tunatarajia kuzalisha ajira kwa watu Mil.1.2

#Natoa wito kwa wahusika wote kusimamia vizuri mradi huu kwani licha ya nchi na taasisi nyingi kutufadhili, fedha nyingi ni za mkopo hivyo muhakikishe mnasimamia vizuri mradi huu ili malengo ya kukopa fedha hizo yaweze kutimia.

*Waliyoyasema viongozi wengine*

#Natoa rai kwa wanaohusika na Mpango huu kuendelea kuwa na weledi katika kusimamia mpango huu ili kuendelea kupata matokeo bora kama ilivyokuwa katika awamu zilizopita - Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

#Napenda kuwakumbusha Watanzania kuwa TASAF ni mradi wa Serikali, unagharamiwa kwa kutenga fedha katika bajeti za kila mwaka pamoja na kukopa fedha ambazo pia zitalipwa na Serikali hivyo zitumike kwa usahihi - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika.

#Awamu ya tatu ya TASAF kwa upande wa Zanzibar hadi kufikia Oktoba, 2019 imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 4.6 kwa shughuli mbalimbali - Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed.

#Tunajivunia sana kuona maendeleo ya mpango huu wa TASAF yaliyopatikana kwa miaka iliyopita, hasa katika kuwainua wanawake nchini - Muwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Preeti Arora.

#Naipongeza nchi ya Tanzania kwa hatua hii ya kuendeleza mradi huu muhimu unaonyanyua maisha ya watanzania pamoja na kupunguza umaskini nchini - Balozi wa Sweeden, Anders Sjoberg.

#Kupungua kwa umaskini ni hali inayoenda hatua kwa hatua, kasi ya kupungua kwa umaskini nchini inaenda kwa mwendo kasi ambapo hali ya umaskini wa kipato umetoka 34% mwaka 2007, 28.4% mwaka 2012 na kufikia  26.4% kwa mwaka 2018 - Mtakwimu mkuu wa Serikali kutoka (NBS)Dkt. Albina Chuwa.

#TASAF imechangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza umaskini,kwa mwaka 2018 kupitia mpango huo umaskini umepungua kwa 0.2%, ni asilimia kubwa sana - Mkurugenzi NBS, Dkt. Albina Chuwa.

#TASAF ya Awamu ya Tatu ilianza rasmi Februari, 2013 na unatarajia kumalizika mwaka 2023 ambapo kipindi cha kwanza kimekamilika na leo kinazinduliwa kipindi cha pili - Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga.

#Kipindi cha kwanza cha awamu hii ya tatu jumla ya shilingi Trilioni 1.46 zimetumika ambapo utekelezaji wake umefanyika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 159 na katika Serikali ya Zanzibar utekelezaji umefanyika katika wilaya zote - Ladislaus Mwamanga.

#Utekelezaji wa kipindi cha kwanza cha Awamu ya Tatu umeleta manufaa makubwa kwani zaidi ya Kaya maskini Mil.1.1 zenye jumla ya watu 5,296,470 zilipatiwa ruzuku - Ladislaus Mwamanga.

#Wanafunzi zaidi ya Milioni 1.8 waliandikishwa katika Shule za Msingi, wanafunzi 448,409 Shule za Sekondari na wanafunzi 277 waliomaliza kidato cha 6 walipata mikopo ya kujiunga na Vyuo Vikuu nchini - Ladislaus Mwamanga.

#Jumla ya Kaya 253,117 zilishiriki katika miradi inayotoa ajira za muda, miradi 8809 yenye thamani ya sh. Bilioni 130 iliibuliwa na kutekelezwa na jamii - Ladislaus Mwamanga.

#TASAF ya Awamu iliyopita imewanufaisha sana wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo jumla ya mitaa 304 kati ya mitaa 564 imenufaika na fedha zitolewazo na mpango huo - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO*


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.