Na Elinipa Lupembe.
# Katibu Mwenezi chama cha Mapinduzi CCM comredi Hamphray Polepole amefanya ziara ya siku moja na kutembelea miradi mitatu katika kata ya olturumet, Oldonyowas na Ilkiding'a, halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.
# Katika ziara hiyo, Katibu Mwenezi huyo, ameridhishwa na utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika hsmashauri ya Arusha hasa katika utekelezaji wa miradi ya Maenfeleo kisekta.
#Amewapongeza wananchi wa Halmashauri ya Arusha hususani, wananchi wa Kijiji cha Oldonyowas kata ya Oldonyowas kwa kushiriki kuchangia uanzishwaji wa shule mpya ya Sekondari Oldonyowas kwa wananchinhao kujenga vyumba viwili vya madarasa kwa kushirikiana na ANAPA, ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi pamoja na ujenzi wa maabara za masomonya Kemia na Biolojia.
#Ameahidi serikali kuanza kutengeneza barabara ya kuingia katika hospital ya Wilaya ya Olturumet kuanzia eneo la Habari Maalumu kwenye barabara ya Arusha Namanga. Ameahidi kuanza kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe na baadaye kiwango cha lami.
#Amekabidhi gari la wagonjwa wa dharura Ambulance hospitali ya wilaya ya Olturumet na kufutia kodi ya kuingiza gari hilo, gari ambalo lilitolewa msaada na kundi la Friends of German la nchini Ujerumani.Magari ambayo yalizuiliwa kwa kudaiwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, huku taratibu za kufuta kodi hizo ukifuatwa.
#Ametoa zawadi ya jozi mbili za jezi za wachezaji wa mpira wa miguu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza, waliojiunga kwenye shule mpya, ya sekondari Oldonyowas kwa lengo la kuanzisha timu ya mpira wa miguu katika shule hiyo.
#Amefafanua umuhimu wa ziara hiyo kichama, ni kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Ilanibambayo iliwapa nafasi kupata dhamana ya kuongoza nchi kwa kipindibcha miaka mitano.
#Amewataka wananchi kutambua na kutofautisha siasa na kazi na kufahamu kuwa, ziara ya chama tawala kilichoko madarakani, inalengo la kuhakikisha kile ilichowaahidi wananchi ndio kinatekelezwa na si mikutano ya kujenga chama, kama inavyotafsiriwa.
#Amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli inaendesha siasa za maendeleo za kuwahudumia wananchibkwa vitendo kwa kufikisha huduma za jamii hasa kwa wananchi waishio vijijini.
#Katika ziara hiyo, Katibu Mwenezi huyo aliambatana na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Arusha, wilaya ya Arumeru na viongozi mbalimbali wa chama kuanzia ngazi ya mtaa, kijiji, kata, wilaya, mkoa na taifa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.