Na Elinipa Lupembe
# Waheshimiwa madiwani wameiomba Serikali Kuu kushirikiana na halmashauri kupanga upya utaratibu wa kugawa shamba la Tanzania Plantations kwa kuzingatia maslahi mapana ya halmashauri na wananchi wake, kutokana na kutoridhishwa na utaratibu uliowasilishwa na Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa kupanga matumizi ya shamba hilo, mara baada ya kuwasilishwa taarifa ya Wizara ya Ardhi ya kupanga matumizi ya ardhi katika shamba hilo.
#Wamempongeza Mkururugenzi Mtendaji na timu ya watalamu kwa kufikia 95% ya ukusanyaji wa mapato hadi tarehe 30 Juni 2022 jambo ambalo halijawahi kutokea, na kwasisitiza kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato na usimamia thabiti na kufikia 100% kama ilivyo kwa halmashauri nyingine.
# Waheshimiwa Madiwani, wametakiwa kushirikiana na watalamu kubuni vyanzo vya mapato pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa vyanzo vilivyo kwenye maeneo yao, kwa pamoja halmashauri itaimarika kimapato.
#Waheshimiwa Madiwani kuendelea kuhamasisha wananchi katika maeneo yao, kushiriki Sensa ya watu na makazi, itakayofanyika tarehe 23.08.2022 ili zoezi hilo lifanyike kwa ufanisi na kuhakikisha watu wote waliolala kwenye kata zao wamehesabiwa.
# Kuendelea kusimamia utekelazaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenya vijiji na kata na kuhakikisha miradi hiyo imekamilika kwa wakati na kuhakikisha viwango vya ubora unaozingatia thamani ya pesa zilizotumika.
ARUSHA DC TUPO TAYARI KUHESABIWA
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022
PICHA ZA MATUKIO MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.