*Yalojiri wakati wa ziara ya Katibu mkuu ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Joseph Nyamuhanga Arusha DC., Alipozungumza na wanafunzi na watumishi wa shule ya Sekondari Ilboru*
#Amekagua mradi wa ukarabati wa shule ya sekondri ya Ilboru, ikiwemo vyumba vya madarasa, vyoo, maabara za masomo ya Sayansi, jengo la utawala, holi la kusomea, uligharimu kiasi cha shilingi bilioni 1,06 fedha zilizotolewa na serikali kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
#Amewataka wanafunzi wa shule hiyo kuongeza bidii katika masomo na kuweza kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa kwa kufuta alama 0 na IV na kuweza kuwashinda wanafunzi wa shule binafsi.
#Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano, imekuwa ikitoa kiasi cha shilingi bilioni 288.5 kwa mwaka, sawa na shilingi bilioni 24.04 kwa mwezi na shilingi milioni 600 kwa kila wilaya, kwa ajili ya elimu bila malipo, lengo likiwa ni kutoa fursa sawa kwa watoto wa kitanzania kusoma, pamoja na kuwapunguzia wazazi mzigo wa kulipa ada, hasa watoto wa familia duni.
# Serikali imeboresha kwa kukarabati jumla ya shule kongwe 46 Ilboru ikiwemo na kuwataka wanafunzi hao kutumia fursa hiyo kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanapata daraja la kwanza na la pili tu, kutokana na ubora wa miundombinu ya shule na mazingira rafiki ya kujifunzia.
#Ameahidi kutafuta fedha kwa ajili ya gari la shule hiyo pamoja na kumalizia ukarabati wa majengo ambayo bado yanahitaji ukarabati ikiwemo ukumbi wa mikutano.
# Ameahidi kukarabati nyumba za awalimu wa shule hiyo, kutokana na uchakavu wa nyumba hizo uliotokana na kujengwa miaka mingi iliyopita, ili wawezeshe kuishi katika mazingira bora.
#Amewataka walimu, kuongeza juhudi katika ufundishaji kwa kutenga muda kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambao kimsingi uwezo wao ni mdogo ili kuondoa daraja 0 na IV katika shule hiyo.
#Ameiagiza Wakala wa barabara - TARURA, halmashauri ya Arusha, kufanya makisio ya matengenezo ya barabara ya kuingia shule ya sekondari Ilboru ili iweze kutafutiwa fedha kwa ajili ya ukarabati huo.
#Amepongeza uongozi wa Wilaya ya Arumeru na halmashauri ya Arusha kwa usimamizi imara uliyowezesha matumizi ya fedha za serikali kiasi cha shilingi bilioni 1.06 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya shule ya sekondari Ilboru.
#Ameipongeza Jumuia ya Ilboro kwa kufanyakazi kwa bidii na kuwawezesha wanafunzi wa shule hiyo kufanya vizuri kwenye mitihani ya taifa na kuwa kwenye shule 20 bora na kutoa wanafunzi wanaoshika nafasi ya kumi bora kitaifa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.