Zaidi ya shilingi milioni 90 zatumika katika mradi wa ujenzi wa vyoo bora kwenye masoko ya Kata za Oltrumet na Olmotonyi kwa ufadhili wa Shirika la WaterAid chini ya mradi unaotekelezwa na Habitat for Humanity.
Akizungumza kuhusu manufaa ya mradi huo kwa jamii, Meneja wa msimamizi wa mradi toka Shirika la WaterAid bwana Charles Bujashi amesema kuwa mradi huo wa vyoo bora katika masoko utahudumia zaidi ya wamama elfu moja wanatoa huduma za kuuza bidhaa mbalimbali kwenye masoko ya ngaramtoni.
Bwana Bujashi amesema kuwa wakati zoezi la ujenzi likiendelea, Watalaamu hao toka WaterAid walikuwa na kazi ya kutoa elimu kwa vikundi 21 vya wanawake toka masoko ya Kata za Oltrumet na Olmotonyi kuhusu elimu ya ujasirimali, uongozi na elimu ya fedha ili kuwawezesha kufanya ujasirimali kisasa kwa lengo la kuwaletea kipato zaidi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.