• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Zaidi ya watu 400 wajitokeza kutibiwa macho kwenye maazimisho ya siku ya macho Duniani

Posted on: October 12th, 2018

Zaidi ya watu 400 katika halmashauri ya Arusha,wilayani Arumeru wamepata huduma ya mbalimbali matibu ya macho, katika zoezi la  upimaji wa macho lililofanyika kwa wa siku nne mfululizo, kueleea kilele cha maazimisho ya siku ya Huduma za Macho Duniani, maazimisho yaliyifanyika kimkoa katika kituo cha afya cha nduruma wilayani humo.

Zoezi hilo la  matibabu ya macho limepokelewa kwa mwitikio mkubwa na wananchi wa kata ya Nduruma na vitongoji vyake, pamoja na kata za jirani za mlangarini na Bwawani kutokana  na huduma hiyo  kutokupatikana katika maeneo hayo.

Akifunga kilele cha maadhimisho hayo, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, Afisa Tawala wa wilaya hiyo, Mushashu Anaclet amesema kuwa, licha ya huduma za macho zinazotolewa katika viwanja hivyo lakini  lengo kuu la  maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kutunza macho ili kuepuka upofu unaozuilika pamoja na kuonyesha hali  halisi ya magonjwa ya macho nchini na duniani.

Ameongeza kuwa takwimu za magogonjwa ya macho kwa mkoa wa Arusha mwaka 2017, zinaonyesha kuna tatizo la  mtoto wa jicho  kwa asilimia 90, shinikizo la  jicho asilimia 2 na tatizo la   trakoma lipo kwa asilimia1.2, huku halmashauri ya Arusha vijijini ikikabiliwa na tatizo la   mtoto wa jicho kwa asilimia 27, kovu kwenye kioo cha jicho asilimia 35 na trakoma asilimia 1.

Aidha Anaclet amewashauri wananchi k,uacha kutumia mitishamba kutibu macho, badala yake  wafike kwenye vya kutolea huduma ya ayfya pindi wanapohisi wana matatizo ya macho, kwani imegundulika kuwa, miti shamba inaweza kusababisha makovu kwenye kioo cha jicho na hatimaye kusababisha upofu.

"Niwashauri wananchi wenzangu acheni kutumia miti shamba kutibu matatizo ya macho miti shamba inasababisha makovu ambayo mwisho wake yanasababisha upofu, nendeni hospitali  mkatibiwe na wataalamu kupitia vipimo vya kisasa na  upatiwa vipimo sahihi kulingana na tatizo ulilonalo msicheze na jicho kwani jicho nikiungo kisicho na mbadala" amesema mgeni rasmi huyo.

Hata hivyo amewataka wale wenye  uhitaji wa miwani kwaajili ya kuona  vizuri waende katika hospitali  zilizosajiliwa ili wafanyiwe vipimo sahihi na kupewa miwani kulingana na vipimo vyao na sio kupata huduma mitaani.

Naye Mratibu wa macho na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, mkoa wa Arusha Dkt. Mwanahawa Kombo amesema kuwa zoezi hilo limepata mafanikio makubwa, kwani walilenga kutoa matibabu kwa wananchi 200 badala yake, kumekuwa  na mwitikio mkubwa  hadi  sasa tayari wametibiwa  wananchi takribani 400 jambo ambalo limesababisha kuvuka malengo.

Aidha amezitaja huduma za macho zinazotolewa kituoninhapo ni pamoja na kupima macho, kutoa dawa kwa wale wenye kuhitaji tiba, kupima macho kwa wagonjwa wa kisukari, kufanya upasuaji mdogo wa vikope, kutoa miwani kwa watu wazima kuanzia miaka 40 na kuendelea kwa ajili ya kuonea karibu, kutoa ushauri kwa wagonjwa, sambamba na kutoa rufaa kwenda hospitali ya rufaa KCMC kwa wagonjwa ambao wanahitaji huduma za matibabu zaidi.

Hata hivyo Dkt.Mwanahawa amethibitisha kuwa wagonjwa ishirini, waliogundulika na tatizo la  mtoto wa jicho, watafanyiwa upasuaji katika hospitali  ya St. Elizabeth kwa ufadhili wa shirika la  Kilimanjaro Center for Community Ophthalmology (KCCO) huku wagonjwa wengine waliokutwa na ugonjwa wa vikope wakitolewa pale pale.

Ameongeza kuwa licha ya kujikita zaidi kwenye matibabu ya macho lakini pia wananchi wamepata fursa ya kupima magonjwa mengine ikiwemo kisukari,shinikizo la damu, virusi  vya UKIMWI pamoja na kansa  ya matiti kwa wanawake.

Kwa upande wao wananchi waliopatiwa huduma hiyo  wameipongeza serikali ya awamu ya tano  inayoongozwa na Rais  John Pombe Magufuli,  kwa kuwajali wananchi wake hasa  waishio vijijini, na kuwapelekea huduma hiyo ya matibabu ya macho  huduma ambayo haijawahi kupatikana katika eneo hilo.  

Joshua Lekeiya mwananchi wa kijiji  cha maji moto baada  ya kupimwa na kupatiwa miwani ya kusomea amekira kufurahishwa na huduma hiyo  iliyoletwa karibu nao na kuipongeza serikali ya awamu ya tano  kwa kusema kuwa wananchi wengi sasa hasa  wa vijijini wanapata huduma nyingi  tofauti na hapo  awali walikuwa wakizisikia tu zikitolewa mjini.

"Kiukweli sisi wananchi wa hali  ya chini tunafurahishwa sana na kitendo cha serikali kutuletea huduma hadi  vijijini, Mimi sikuamini kama ni kweli lakini nimefika hapa kituo chetu cha nduruma nimepimwa macho na nimepewa Miwani ya uoni hafifu na nimeshudia wenzangu wakipata huduma mbalimbali za afya ya macho" .amesema Lekeiya

Siku  ya Afya ya macho duniani huadhimishwa kila  alhamisi ya pili ya mwezi wa kumi na katika mkoa wa Arusha maazimisho yamefanyika katika kata ya Nduruma,  halmashauri ya arusha wilayani Arumeru yenye kauli mbiu ya Kauli mbiu 'Afya ya macho kwa wote huduma za macho popote ulipo'.


*PICHA ZA MATUKIO KWENYE KILELE CHA SIKU YA MACHO DUNIANI* 






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.