Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wamefanya ziara ya siku mbili ya kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa ndani ya halmashauri kwa mwaka huu wa fedha 2016/2017.
Katika ziara hiyo wajumbe wa Kamati ya Fedha wametembelea na kukagua jumla ya miradi 20 katika kata za Kiutu, Sokon II, Moivo, Olturoto, Ilboro, Oltrumet, Mwandeti, Musa, Matevesi na Bwawani na kujionea utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na kufanya kikao cha majumuisho ya ziara hiyo..
Wakizungumza wakati wa kikao cha majumuisho Wajumbe hao licha ya kuridhishwa kwa aslimia kubwa ya utekelezaji wa miradi hiyo waliuagiza uongozi wa halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia weledi na ubora wa miradi unaoendanana thamani halisi ya fedha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.