Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango,halmashauri ya Arusha, wamefanya ziara ya kukagua shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya nne ya kufunga mwaka wa fedha 2018/19.
Miradi ilityotembelewa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Likamba kata ya Musa, ujenzi unaohusisha jumla ya vyumba 4 vya madara, vyoo na nyumba ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia 8 (8in1) kupitia michango ya wananchi wa kijiji cha Likamba, ujenzi wa ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule, fedha za Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi, ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Sokon II kwa ufadhili wa Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, kukindi cha wanawake Ilboru kilichopewa mkopo wa aslimia 4 ya mapato ya ndani, na eneo la uwekezaji Engira.
k
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.