Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wamefanya ziara ya siku tatu ya kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri ya Arusha kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa kipindi cha robo ya tatu ya kuanzia mwezi Oktoba mpaka Disemba 2017.
Wajumbe hao wametembelea na kukagua jumla ya miradi 20 yenye thamani ya shilingi milioni 822.4 kwenye kata 27 za halmashauri hiyo na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uendelezwaji na utekelezwaji wa miradi hiyo.
Wajumbe hao wameridhishwa na kwa aslimia kubwa ya utekelezaji wa miradi hiyo hasa miradi iliyotumia 'Force Akaunti' njia inayotumia gharama nafuu, muda mfupi pamoja na ushirikishwaji wa wananchi kwa kutumia local fundi wa eneo husika.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.