Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Missaile Musa ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Arusha na kupongeza Uongozi kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi hiyo ambayo imekidhi viwango kwakuonyesha thamani halisi ya fedha iliyotumika.
Katika ziara hiyo Katibu Tawala Mkoa alipata fursa ya kutembelea Shule ya sekondari Kiutu ambapo alikagua jengo la nyumba ya Mwalimu 3 in 1, Shule ya sekondari Mlinga, Moivo sekondari, Lemayan shule ya msingi pamoja na kituo cha Afya Oldonyosambu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.