Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mheshimiwa Dk. Hamis Kigwangala amefanya ziara ya siku mbili katika halmashauri ya Arusha na kukagua Vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya ya Olturumet na kujionea huduma za afya zinavyotolewa.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri ametembelea vituo vitatu vya Afya ikiwemo kituo cha Afya cha Oldonyosambu, Olkokola na Nduruma pamoja na hospitali ya halmashauri ya Wilya ya Arusha Olturumet iliyoko katika kitongoji cha Ekenywa kata ya Olturumet mkabala na Redio Habari Maalumu takriban mita mia tatu kutoka barabara ya Arusha-Namanga.
Naibu Waziri Dk. Kigwangala licha ya kuridhishwa na juhudi zilizofanywa na halmashauri ya Arusha za kuhakikisha upatikanaji rahisi wa huduma za afya kwa wananchi ametoa wito wa kuboresha vituo hivyo pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.