Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha,bwana Seleman Msumi ( mwenye kofia) akiwa ameambatana na Meneja wa Soko la Machinga Jijini Dodoma( Machinga Complex) bwana Faustine Masanja, ikiwa ni ziara ya mafunzo ya Madiwani na Wataalam toka Halmashauri ya Arusha.
Lengo la ziara hiyo ya Madiwani na Wataalam toka Halmashauri ya Arusha ni kujifunza na kupata uzoefu wa kubuni vyanzo vipya vya mapato,kudhibiti mapato pamoja kuanzia miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia mapato ya ndani.
Katika ziara hiyo Madiwani na Wataalam walipata wasaha wa kutembelea mradi wa uwekezaji wa Hoteli ya kisasa inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na soko la Wafanyabiara wadogo( Machinga Complex) lililopo makutano ya barabara ya Bahi na Arusha
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.