Madiwani wa Halmashauri ya Arusha wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Dkt.Ojung'u Salekwa wameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa uwekezaji mkubwa wa miradi mbalimbali ambayo ni chanzo kikubwa cha mapato kwa Jiji hilo
Wakiwa katika ziara ya mafunzo Jiji hapo, Madiwani hao leo tarehe 20/12/2024 wamepata fursa ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Jiji hilo ikiwemo Hotel na ukumbi wa mikutano unaweza kuketisha watu 1000 kwa wakati mmoja uliopo Mji wa Serikali Mtumba, soko la kisasa la Job Ndugai, Stendi ya Kisasa ya Mabasi ya abiria, mradi wa maegesho ya malori ta mizigo eneo la Nala pamoja na
Pamoja na pongezi hizo,Madiwani hao wamehaidi kwenda kutekeleza miradi ya Kimkakati waliyokwisha ibuni ikiwepo ujenzi wa Hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota 5 ambapo michoro yake imekwisha kamilika ikizingatiwa kuwa Arusha ni Mkoa wa Utalii na Mikutano ya Kimataifa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Oltroto, Mhe.Baraka Mesiaki amesema ni wakati sasa Arusha iwe na Miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa mradi wa stendi kubwa ya Mkoa ya Kisasa,Masoko malubwa katika maeneo ya miji ya Ngaramtoni, maegesho makubwa ya malori kwenye barabara ya Arusha kwenda Namanga katika Kata ya Oldonyowasi ambapo kuna maeneo makubwa ya wazi.
" Nadhani ifike mahali tufanye maamuzi magumu kama yaliyofanya na Serikali Kuu ya kuhamia Dodoma, haikuwa rahisi kuhamishia Wizara zote kwa mara moja kutoka Dar Es salaam kuja Dodoma, leo tumeona mji wa Serikali Mtumba ulivyopendeza,hivyo nasi Arusha DC lazima tukatengeneze historia,hatuna muda wa kupoteza tena wacha tufanye mambo kwa maslahi ya wananchi wetu" alisema Mhe.Baraka
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.