Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha akikabidhi mbuzi wa maziwa 165 kwa vikundi kumi vya kaya masikini 155 katika kijiji cha Imbibia kata ya Mwandeti ikiwa ni utekelezaji wa mradi ya OPEC miradi inayotekelezwa na TASAF awamu ya tatu.
Bibi Nasieku Molel mkazi wa kijiji cha Ilkiushini kata ya Oltrumet akimsimulia Afisa Habari Elinipa Lupembe namna fedha za mpango wa kunusuru kaya masikini zilivyomnufaisha tangu alipoanza kupokea.
Wakazi wa kijiji cha Laroi wakisafisha eneo tayari kwa kuanza ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya msingi Laroi mradi moja ya miradi ya OPEC inayotekelezwa na TASAF awamu ya tatu, wananchi hao wanatekeleza utaratibu kwa kuchangia mradi huo kwa asilimia kumi.
Wananchi wa kijiji cha Laroi wakichonga miti kwa ajili ya kuanzaujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya msingi Laroi mradi moja ya miradi ya OPEC inayotekelezwa na TASAF awamu ya tatu, wananchi hao wanatekeleza utaratibu kwa kuchangia mradi huo kwa asilimia.
Msanifu wa majengo ndugu Peter Mhina akiwaelekeza wakazi wa kijiji cha Laroi kupima eneo la ujenzi wa nyumba ya mwalimu mardi wa OPEC unaotekelezwa na TASAF awamu ya tatu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.